Je, Unaifahamu Computer?

Katika jamii zetu za Afrika hususan Tanzania, watu wengi wanashindwa kumiliki kompyuta kutokana na hali duni ya maisha, na wengine wengi hawana ujuzi wala utambuzi juu ya kompyuta kutokana na sababu tofauti ikiwemo, kutojua umuhimu wa kompyuta na utambuzi wa lugha ya Kiingereza. Je, unaifahamu Computer? ni kitabu kilicho lenga aina hii ya watu, ambao kwa namna moja au nyengine wanahitaji kujifunza kompyuta ila lugha ya kiingereza imekua ngumu kwao, hawana pesa za kujifunza kompyuta katika taasisi na vyuo mbali mbali vinavyo toa taaluma hii, hawana muda wa kutosha kutokana na kutingwa na majukumu ya kijamii na ya serikali.